Wanaharakati wa upinzani Tanzania walioiteka Twitter

Wafahamu Wanaharakati wa upinzani Tanzania walioiteka mitandao ya kijamii kama vile Twitter, Facebook na Instagram

1. Maria Sarungi Tsehai

Wanaharakati was upinzani Tanzania-maria serungi

Maria Sarungi Tsehai ni mwanaharakati wa Kitanzania anayejulikana kwa kampeni yake mtandaoni “Badilisha Tanzania”. Change Tanzania ilianza kama lebo kwenye Twitter (#changeTanzania) kushawishi raia wa Tanzania kushiriki katika kuleta mabadiliko chanya katika nyanja tofauti za maisha, haswa katika masuala ya kisiasa nchini Tanzania.Anajulikana pia kwa kuwasaidia wanawake wadogo kufikia malengo yao katika tasnia ya mitindo kwani yeye ni mkurugenzi wa miss universe Tanzania.

Maria Sarungi-Tsehai ni mtaalam wa mawasiliano na mhusika wa vyombo vya habari, na vile vile mtetezi wa haki za binadamu na mtetezi wa haki za wanawake na wasichana. Yeye ndiye mkurugenzi na mmiliki wa Compass communication na ameongoza na kutoa filamu na nyaraka kadhaa za kushinda tuzo.

2. Fatma Karume aka Shangazi

Wanaharakati was upinzani Tanzania- fatma karume

Fatma Karume (amezaliwa 15 Juni 1969) ni mwanasheria wa Kitanzania na wakili wa kujitegemea, mwanaharakati ambaye aliwahi kuwa rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) katika kipindi cha mwaka 2018 hadi 2019. Alipata wadhifa huo baada ya kushinda katika uchaguzi wa uraisi wa chama hicho uliofanyika Aprili 2018 na hivyo kumrithi mtangulizi wake Tundu Lissu aliyekiongoza chama hicho kutoka mwaka 2017 hadi 2018

Maduka 4 bora ya kununua bidhaa mtandaoni-Tz

Fatma ni mjuzi wa sheria zinazohusiana na mizozo ya ushuru, mizozo ya wafanyikazi na ana rekodi ya kufanikiwa kuwakilisha benki za ngazi za juu katika madai ya kibiashara na usuluhishi pamoja na ukaguzi wa kimahakama, mizozo ya ushuru, ufilisi na upokeaji, sheria ya mali miliki, na sheria ya media
Amekuwa na ushawishi mkubwa kwenye mtandao wa Twitter ambapo amejizolea followers 592k.  Pia amekuwa rafiki wa wafuasi wa vyama pinzani kutokana na msimamo wake wa kuunga mkono harakati za upinzani katika kukiondoa chama tawala.

“Natafakari lakini nataka mabadiliko, hilo I will never give up on (sitolikatia tamaa). Hatuwezi kuishi kwenye nchi iliyokuwa na dhuluma kiasi hiki.” — @fatma_karume, Sept 2019

Baadhi ya matukio aliyokumbana nayo hivi karibuni ni pamoja na kuvuliwa uwakili na kutishiwa aman.

Madau wa jamiiforum anauliza Hivi kinachofanya Maria Sarungi na Fatma Karume wawe wanaharakati namna ile ni nini?

3. Kigogo

Wanaharakati was upinzani Tanzania -kigogoHuyu ni mwanaharakati aliejizolea umaarufu kutokana na juhudi za kufichua siri za serikali. Amekuwa akificha uhusika wake kwa muda mrefu hivyo kupelekea kutofahamika na mtu yeyote, kwani hata jeshi la polisi lilipotangaza dau nono kwa atakaemfichua hadi sasa hakuna alietangazwa kujitokeza kumfichua.

Amekuwa na ushawishi mkubwa kwa wanachama na wafuasi wa vyama pinzani kwa kwenye mtandao wa Twitter ambapo amejizolea followers takribani laki tano na ishirini na tano (525k)
Baadhi ya mambo yaliyomwongezea umaarufu hivi karibuni ni pamoja na suala la kutumia VPN katika kipindi cha uchaguzi mkuu 2020 na Kufichua wagonjwa wa corona.

4. Zibwabwe

Roma mkatoliki

Zimbabwe au maarufu kwa jina la Roma mkatoliki ni mwanaharakati na pia mwanamziki wa bongo fleva aliyejizolea umaarufu kutokana na kufanya harakati kwa njia ya mziki. Amekuwa akiimba nyimbo nyingi za kufichua na kukosoa matendo ya serikali.

Roma mkatoliki aliwahi kutekwa na watu wasiojulikana mwaka 2017 na kuachiwa huru ambapo ili kunusuru maisha aliamua kukimbilia nje ya nchi na ndio anakoishi mpaka sasa.

5. Ansbert Ngurumo

Ansbert ngurumo

Mwandishi wa habari mwandamizi ambaye amefanya kazi na vyombo kadhaa vya habari nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na gazeti la Mwanahalisi. Ngurumo ambaye amekimbilia ulaya nchini Finland kwa kile anachokiita kuwa ni kunusuru maisha yake.

Ngurumo: Kimsingi yaliyonikuta ni marefu sana lakini la msingi ni kuwa nimekimbia, nimejificha najihadhari na ni tofauti na wanaosema nimeikimbia nchi, mimi sijaikimbia nchi, nchi ni ya kwangu, mimi ni mtanzania na najua mambo haya yataisha na nitarudi. Lakini kitu kikubwa ni kwamba nimewakimbia wauwaji, nimekimbia watesaji , nimekimbia watu wanaowateka watu ambao wanalindwa na dola..Aliongea hayo akihojiwa na BBC

“Ingawa sipo huko, najua kinachoendelea Tanzania na nitaendelea kuandika kuhusu nchi yangu, kinachonifanya niwe hapa (Finland), nataka kuwa hai. Ninawaomba,”amefahamisha na kuwaasa waandishi wa habari kujihadhari. Akiongea na RFI Kiswahili

6. Martin M.M

Maltin m.m

Maltin M.M ni mwanaharakati anayeunga mkono juhudi harakati za wanaharakati wengine. Ni mwanaharakati wa upinzani anayefatilia kwa kina matukio ya vyama vya upinzani na chama tawala na kukosoa pale jambo fulani kuonekana haliko sawa.

Katika tweet yake ya hivi karibuni

“Natafakari lakini nataka mabadiliko, hilo I will never give up on (sitolikatia tamaa). Hatuwezi kuishi kwenye nchi iliyokuwa na dhuluma kiasi hiki.” — @fatma_karume, Sept 2019

Shangazi Fatma, maneno hayo yananibariki mara zote. Heri ya siku ya kuzaliwa. Miaka 52. Bado kijana✌️ https://t.co/lWzlIWxv6W

7. Goodluck

Goodluck

#RealGoodluckHaule ni mwanaharakati wa kujitegemea aliyejizolea umaarufu kutokana na harakati zake za kukosoa matendo ya serikali yanayovunja sheria na haki za binadamu. Baadhi ya tweets zake za hivi karibuni ni:

The main purpose of Activism is to promote, impede, direct, or intervene in social, political, economic, or reforms with the desire to make changes in society toward a perceived greater good. That’s what @RealHauleGluck are doing; we ain’t anarchist or anti-government!

8. Think Different

Think different

Ni mwanaharakati wa upinzani kwenye mtandao wa twitter anayejihusisha na masuala ya haki za binadamu. Amekuwa akikosoa serikali kwenye mwenendo wa uvunjifu wa haki za binadamu. Mfano wa tweet yake ya hivi karibuni ni:

Tulioonza kampeni ya #Justice4Uamsho kuna watu walituambia nyie kama NGO namshiriki mambo ya dini mambo ya kigaidi

Moja ya tatizo tulilonalo ni ubinafsi , tuna unafiki mkubwa sana, Leo hawa watu wameachiwa bila Kesi, @moodewji waombe Radhi, you have a tweet judging them https://t.co/KbXIVq8HR2

Andika wanaharakati wengine unaowafahamu kwenye sehemu ya comment hapo chini

Msomeni Blogu

Najihusisha na masuala ya kimtandao, mbinu mbalimbali za kuanzisha na kuendeleza biashara ya mtandaoni. Email yangu ni msomeniblogu@gmail.com au WhatsApp namba ni 0718453258

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

© 2021 MSOMENI BLOG - Theme by WPEnjoy · Powered by WordPress