Usiombe ufundishe Chekechea utajuta

Dada wa kazi kidogo amtoe roho bosi wake

Dada wa kazi za ndani alimfata mke wa bosi na kuomba aongezewe mshahara.
Mke wa bosi alishangazwa sana na kitendo cha dada wa kazi huyo kwani hajaona kazi ya ziada inayofanywa na dada huyo hadi atake kuongezewa mshahara.

Mke: Kwanini unataka kuongezewa mshahara

Dada wa kazi: mimi napika vizuri sana kuliko wewe.

Mke: Nani aliekuambia hivyo

Dada wa kazi: Mumeo ndio kaniambia hivyo

Mke: Oh!

Dada wa kazi: Sababu ya pili ni kuwa mimi napiga pasi nguo vizuri kuliko wewe.

Mke: Enhe nani tena aliekwambia hivyo?

Dada wa kazi: Mume wako

Mke: oh!

Dada wa kazi: Na sababu ya tatu, mimi niko vizuri kwenye tendo la ndoa kuliko wewe.

Mke: Ahaa ni mume wangu uyo amekwambia si ndio! 😐😐

Dada wa kazi: Hapana, ni Juma mlinzi wa getini ndo ameniambia hivyo.

Mke: ahaa ☺☺ unataka nikuongeze sh ngap? 😂😂😂

 

USIOMBE UFUNDISHE CHEKECHEA

 

Mwalimu Sofia alikuwa darasani anafundisha somo la kuhesabu kwa wanafunzi wa Chekechea

Mwalimu: Kama nitakupa mbwa wawili, nikaongeza tena wawili alafu nikaongeza wengine wawili, jumla utakuwa na mbwa wangapi?

Junior: Mbwa saba

Mwalimu: Hapana junior, sikiliza kwa makini narudia swali, “Kama nitakupa mbwa wawili, alafu nikaongeza tena mbwa wawili kisha nikaongeza tena wengine wawili” Jumla utakuwa na mbwa wangapi?

Junior: Mbwa saba

Mwalimu: Oh hapana, ngoja niweke swali kwa mtindo mwingine, “Kama nitakupa pipi mbili, nikakupa tena pipi mbili alafu nikaongeza pipi nyingine mbili, jumla utakuwa na pipi ngapi?

Junior: Pipi sita

Mwalimu: Safi sana, enhe turudi kwenye swali letu. Kama nitakupa mbwa wawili, alafu nikaongeza tena mbwa wawili kisha nikaongeza tena wengine wawili, jumla utakuwa na mbwa wangapi?

Junior: Mbwa Saba

Mwalimu: oh wewe Junior hao mbwa saba unawapataje?

Junior: Mbwa wangu mwingine yuko nyumbani kanipa baba. 😂😂😂

KUPATA Vichekesho zaidi bonyeza hapa

Tembelea Facebook page yetu hapa Msomeni blog

MWISHO

Related Posts

Msomeni Blogu

Najihusisha na masuala ya kimtandao, mbinu mbalimbali za kuanzisha na kuendeleza biashara ya mtandaoni. Email yangu ni msomeniblogu@gmail.com au WhatsApp namba ni 0718453258

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

© 2021 MSOMENI BLOG - Theme by WPEnjoy · Powered by WordPress