Ukiona dalili hizi jua simu yako imedukuliwa

Ukiona dalili hizi za hatari ujue simu yako imedukuliwa. Taarifa zako sio za siri tena, kuna mtu anaona kila kitu kwenye simu yako.

Simu yako imedukuliwa

Ni muhimu sana kuhakikisha simu yako inatunza siri zako na hakuna mtu mwingine anaweza kufikia au kusoma taarifa zako. Hii ni kwasababu mtu akiweza kupata taarifa zako za siri kwenye simu yako ataweza kufanya uhalifu wowote kama vile kuiba pesa kutoka kwenye akaunti ya benki iliyounganishwa na simu yako, Tigo pesa n.k. na taarifa nyingine za muhimu ikiwemo kudukua akaunti yako ya mitandao ya kijamii.

Jinsi ya kuuza bidhaa mtandaoni kwa haraka

Hivyo ni lazima kuwa makini na simu yako ili kuepusha athari zozote za kudukuliwa. Wadukuzi hutumia mbinu mbalimbali kudukua simu yako kama vile kukutumia link na ukibonyeza tu utakuwa ume-install vidukuzi.

Pia wadukuzi hutumia njia ya ku-install app kwenye simu yako bila wewe kujua na hautaweza kuiona kwenye orodha ya apps zote kwani inakuwa imefichwa. Epuka kumpatia kila mtu simu yako.

Simu yako imedukuliwa kama utaona dalili zifuatazo

1. Kupokea taarifa (notifications) za app ambayo hauitumii

Hii ni dalili kuwa simu yako ina app ambayo kuna mtu ame-install kwa siri kwa lengo la kudukua au kuiba taarifa zako. Pia labda ulibonyeza link mtandaoni ambayo ikafanya installation ya app bila wewe kujua. Ukiona hivyo angalia Kama sehemu ya ulinzi wa apps zote kwenye simu yako iko ‘ON’

⛔ Ingia playstore kisha bonyeza alama ya duara la blue upande wa juu kulia

Simu yako imedukuliwa, wezesha ulinzi playstore

 

⛔ Kisha Bonyeza Play protect baada ya kufunguka

Simu yako imedukuliwa, wezesha ulinzi

 

⛔ Bonyeza alama ya ‘Setting’ upande wa kulia juu.

Playstore

 

⛔ Baada ya hapo angalia kama sehemu zote mbili za ulinzi ziko ‘ON’.

Playstore

⛔ Kama hazikuwa ‘ON’ weka ‘ON’ na baada ya sekunde chache playstore ita-scan simu yako na kukuletea taarifa kuwa kuna app sio salama na utatakiwa kui-remove au ku-unistall. Kama sehemu zote mbili ziko ‘ON’ na app imeweza kuingizwa kwenye simu yako suluhisho ni ku-reset au ku-restore simu yako.

2. Kuona meseji zimesomwa bila wewe kuzifungua

Ukiona meseji mara kwa mara kwenye simu yako tayari zimeshafunguliwa na kusomwa bila wewe kufanya hivyo ujue tayari kuna mtu anasoma meseji zako. Cha kufanya restore simu yako au badili namba Kama meseji ni za WhatsApp, badilisha neno la siri kama meseji ni za Facebook na piga simu huduma kwa wateja kama ni meseji za kawaida kwenye laini yako. Jinsi ya kutengeneza blog ya WordPress bure

3. Simu yako kutumia data (MB) nyingi kila ukiwasha data.

Kama simu yako inatumia Mb nyingi na wakati matumizi yako ni ya kawaida anza kuwa na wasiwasi kwa maana huenda kuna app mtu ameinstall kwa siri na inafanya kazi muda wote kufungua mafaili yako. Cha kufanya ingia kwenye ‘Setting’ kisha weka ‘data limit’ na weka ‘OFF’ matumizi ya data kwenye background kea apps zote.  Ukiona matumizi bado yanakuwa makubwa na wewe hutumii sana internet ujue simu yako imedukuliwa.

4. Kutakiwa ku-login muda mfupi baada ya ku-login

Ikiwa inatokea mara kwa mara baadhi ya apps unazotumia kama vile Facebook, Instagram au twitter kutaka ulogin tena muda mfupi baada ya kulogin ujue akaunti yako kuna mtu ameidukua na anafatilia taarifa zako. Cha kufanya badilisha neno la siri. Jinsi ya kuanzisha duka la mtandaoni bure

5. Kupokea meseji za kubadili neno la siri

Ikiwa unapokea meseji kwenye laini yako au kwenye email za kukutaka kubadili neno la siri kwenye akaunti yako bila wewe kuomba kufanya hivyo ujue kuna mtu anacheza na akaunti yako

MWISHO: Endapo unataka kuingia kwenye akaunti yako kwa kutumia simu ya mtu mwingine tumia CHROME BROWSER, bonyeza nukta tatu zilizopo upande wa juu kulia kisha bonyeza ‘New Incognito tab’. Kufanya hivyo kutasaidia mtu asione taarifa zako baada ya kumrudishia simu yake kwani hakuna taarifa yako yoyote itakayobaki kwenye simu take.

Kwa msaada au maswali tuandikie chini kwenye comment au bonyeza hapa

Related Posts

Msomeni Blogu

Najihusisha na masuala ya kimtandao, mbinu mbalimbali za kuanzisha na kuendeleza biashara ya mtandaoni. Email yangu ni msomeniblogu@gmail.com au WhatsApp namba ni 0718453258

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

© 2021 MSOMENI BLOG - Theme by WPEnjoy · Powered by WordPress