Mahitaji muhimu kwa maisha ya geto

Fahamu mahitaji muhimu kwa maisha ya geto ambayo kila mtu anayeishi geto au kutaka kuishi geto ni lazima awe nayo. Mahitaji haya ni ya kawaida sana ambayo kila mtu anaweza kuyamudu.

Maisha ya geto

Kuishi geto hasa kwa vijana ambao hawajaoa au kuolewa kuna faida na changamoto zake. Moja ya faida ni kuishi bila ya kusumbuliwa na mtu (kama unaishi geto peke yako). Hasara yake ni kuwa kazi zinakuwa nyingi kama vile kupika, kufanya usafi, kuchota maji n.k. Jinsi ya kuuza bidhaa mtandaoni kwa haraka

Katika post hii utapata kujua mambo muhimu ambayo ukiwa nayo geto yatarahisisha maisha yako.

Haya ndio Mahitaji muhimu kwa maisha ya geto

1. Pasi ya umeme

Pasi ya umeme

Pasi ni muhimu kuwa nayo kwa matumizi ya kunyoosha nguo zako, mashuka n.k. Nyoosha vizuri nguo zako, fanya uwe na mwonekano wa kuvutia. Nyosha hadi nguo za ndani kuua vijidudu vya fangasi. Nunua pasi kwa sh30,000/ hadi 50,000/

2. Jaba/Dyaba

Jaba la maji

Hii ni ndoo kubwa ya kutunzia maji. Inafaa sana katika mazingira ambayo kuna changamoto ya maji. Hii itasaidia kutunza maji mengi tofauti na kuwa na ndoo nyingi ambazo zinajaza chumba tu.

3. Jagi la kuchemshia maji/heater/kettle

Mahitaji muhimu geto-heater

Ni jambo la muhimu sana kuwa na jagi la kuchemshia maji ambalo litasaidia katika kuchemshia maji, chai, maziwa n.k. Nunua jagi lako kwa gharama nafuu kati ya Sh20,000 hadi 35,000/

4. Hot pot

Hotpot

Hili ni muhimu sana katika kuhifadhi chakula kiendelee kuwa cha moto muda wote. Hot pot linafaa kuhifadhia chakula ulichopika ili ule baadae au unaweza kuhifadhia chakula ulichonunua kwa mama ntilie. Jinsi ya kuanzisha duka la mtandaoni bure

5. Mashine ya kunyolea

Mahitaji muhimu. Mashine ya kunyolea

Ni muhimu sana kuwa na mashine yako binafsi ya kunyolea tofauti na kutumia nyembe. Nunua mashine ya kutumia umeme au ya kuchaji kwa ajili ya kusafisha ndevu au sehemu za siri, ni bei nafuu tu kuanzia Sh 10,000/ hadi 25,000/. Usipende kutumia nyembe zinatoa vipere na kukuachia weusi, saruni maambukizi mengi.

6. Miswaki na mataulo

Hii ni Muhimu kuwa nayo geto kwa ajili ya wageni wa dharula. Pia inafaa sana endapo mpenzi wako amekuja kulala kwako kwa mara ya kwanza. Hakikisha unakuwa na miswaki mipya hata mitatu. Pia taulo mbili sio mbaya. Njia 10 za kuwa na uume mkubwa

7. Glasi za maji

Glasi za maji ni muhimu sana kuwa nazo geto, tofauti na kutumia kikombe kunywea maji, kutumia kwa matumizi mengine ni bora uwe na glasi kwa ajili ya maji ya kunywa au vinywaji kama juisi na soda na kikombe kwa matumizi mengine ya kuchota maji.

Ipi imekuvutia? 

Tuandikie chini kwenye sehemu ya comment.

Ipi imekosekana? 

Taja mahitaji mengine kwenye sehemu ya comment

MWISHO

Related Posts

Msomeni Blogu

Najihusisha na masuala ya kimtandao, mbinu mbalimbali za kuanzisha na kuendeleza biashara ya mtandaoni. Email yangu ni msomeniblogu@gmail.com au WhatsApp namba ni 0718453258

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

© 2021 MSOMENI BLOG - Theme by WPEnjoy · Powered by WordPress