Maduka 4 bora ya kununua bidhaa mtandaoni-Tz

Biashara ya kuuza na kununua bidhaa mtandaoni imekuwa maarufu sana katika miaka hii ya sayansi na teknolojia. Pia imekuwa ni njia rahisi kwa wauzaji na wanunuaji kwani wauzaji huweza kupata wateja walio mbali na maduka yako. Pia wanunuaji huweza kuokoa muda wa kufata na kutafuta bidhaa madukani.

Nchini Tanzania biashara ya mtandaoni inakua kwa kasi sana kutokana na ongezeko la wauzaji wa mtandaoni kupitia website zao au website za uuzaji wa bidhaa kama vile Jiji na kupatana. Ila wauzaji wengi wameweza kutengeneza blog au website zao na kupokea oda na malipo moja kwa moja kutoka kwa wateja wao kisha kufanya delivery.

kununua bidhaa mtandaoni

Kutokana na ongezeko hili la wauzaji wa mtandaoni, matapeli nao wametumia fursa hii kuwaibia watu kwa kufungua website feki na kujifanya ni wauzaji wa bidhaa na endapo utahitaji bidhaa fulani utaambiwa utume pesa ili wakuletee na ukishatuma pesa wanapotelea mitini.

Jinsi ya kutengeneza blog-(hatua kwa hatua)

Ili kuepuka wizi huu, msomeni blog imefanya utafiti wa kina kuchunguza ni website zipi au wauzaji gani ni wakweli na wa uhakika ambao unaweza kulipia bidhaa na ukaletewa bila ya changamoto yoyote.

Orodha ya maduka ya kununua bidhaa mtandaoni nchini Tanzania

Hii ndio orodha ya maduka ya kununua bidhaa mtandaoni nchini Tanzania ambayo yamefanyiwa utafiti wa kutosha na blog hii.

1. Inalipa online shopping

Kununua bidhaa mtandaoni by Inalipa

Inalipa online shopping ni wauzaji wa bidhaa mtandaoni wenye makao yao jijini Dar es salaam. Hawa ni wauzaji wa uhakika ambao unaweza kulipia bidhaa moja kwa moja kupitia njia mbali mbali za malipo kama vile tigo pesa na ukapokea oda yako haraka.

Pia watoa huduma kwa wateja wanabidii sana ambapo watakupigia simu dakika moja tu baada ya kuweka oda yako. Jambo lingine la uhakika zaidi ni kuwa unapokea ujumbe wa risiti ya uthibitisho wa malipo yako wenye nembo ya mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)

UBORA WAO
  • Wanafanya delivery kwa haraka sana
  • Huduma kwa wateja ni bora
  • Bidhaa zao zina warranty
  • Njia za kufanya malipo ni rahisi (Tigo pesa, M-pesa nk)
UDHAIFU WAO
  • Ukosefu wa bidhaa za aina nyingi kwenye website yao

Tembelea Inalipa hapa

2. Kikuu online shopping

Kununua bidhaa mtandaoni from Kikuu

Kikuu online shopping ni miongoni mwa wauzaji maarufu sana mtandaoni wanaosifika kwa kuuza jumla na rejareja kwa bei ya kiwandani (nafuu). Wanapatikana Dar es salaam lakini wanafanya biashara na watu wote nchini Tanzania.

Unayempenda hakupendi sababu zote hizi hapa

UBORA WAO
  • Bidhaa zao ni bei nafuu
  • Unaweza kuweka oda ya bidhaa ambayo dukani haipo.
  • Wanafanta delivery sehemu zote.
UDHAIFU WAO
  • Mzigo unachelewa kufika(delay delivery)
  • No free delivery

Tembelea Kikuu hapa

3. Kariakoo shopping mall

Kununua bidhaa mtandaoni from kariakoomall

Kariakoomall ni miongoni mwa wauzaji waliojizolea umaarufu mkubwa kutokana na ubora wa huduma zao ambazo zinaambatana na punguzo kubwa la bei.

Pia wanatoa ofa za bei maalumu kwa kipindi fulani cha mwaka kama vile sikukuu za mwaka mpya, Christmas na iddi. Wana mawakala wengi ambao wanafanya shughuli za delivery kuwa nyepesi sana.

Tembelea kariakoomall hapa

4. Emoa online mall

Kununua bidhaa mtandaoni from emoa
Emoa shopping mall ni miongoni mwa wauzaji wa mtandaoni wenye maduka yao Kariakoo jijini Dar es salaam. Ni website inayokuwa kwa kasi sana kutokana na uwaminifu na ubora wa huduma zao.

Emoa wanatoa ofa ya punguzo la bei kama utanunua bidhaa zao mtandaoni tofauti na  kununua moja kwa moja dukani kwao. Wanafanya delivery bure na haraka sana kwa wateja waliopo Dar es salaam.

Njia 10 za kuwa na uume mkubwa

Wana njia nyingi za malipo ikiwemo kutuma pesa kwenye namba yao ya M-pesa au kulipia bidhaa baada ya kuipokea.

Udhaifu wa Emoa ni kwamba website hii ni mpya ambayo imeanzishwa mwezi desemba mwaka 2020 hivyo hakuna bidhaa za kutosha zilizowekwa. Lakini ukihitaji bidhaa unaweza kuwapigia simu na wakakuuzia kwa bei ya mtandaoni kisha  kukuletea sehemu ulipo.

Wateja wa nje ya Dar es salaam wanafurahishwa sana na website hii kwasababu wanapokea bidhaa kwa wakati na kwa uaminifu mkubwa.Msomeni blog tumekuwa tukiagiza bidhaa mbalimbali kutoka kwa Emoa na mzigo unafika kwa uhakika.

Tembelea Emoa hapa

MWISHO: Msomeni blog inaendelea kufanyia tafiti wauzaji wengine na tutakuja na ripoti mpya ya websites za kununua na websites za kuepuka (matapeli).

Weka duka au website yako ya uhakika kwenye sehemu ya comment ili wengine waifahamu

Related Posts

Msomeni Blogu

Najihusisha na masuala ya kimtandao, mbinu mbalimbali za kuanzisha na kuendeleza biashara ya mtandaoni. Email yangu ni msomeniblogu@gmail.com au WhatsApp namba ni 0718453258

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

© 2021 MSOMENI BLOG - Theme by WPEnjoy · Powered by WordPress