Kisa cha kusisimua cha Profesa

Soma kisa cha kusisimua cha profesa huyu aliyeingia darasani na kukutana na tabia mbaya ya mwanafunzi wake iliyopelekea taharuki.

Anza sasa

Profesa alipo ingia darasani alianza na mada nzito sana.
Wakati alipogeukia ubaoni, mmoja wa wanafunzi alipiga filimbi.
Aligeuka, akatazama darasa na akauliza jina la aliepiga filimbi.
Hakuna aliyejibu.

Kisa cha kusisimua
Profesa kwa amani aliweka kalamu mfukoni akasema:
“Tuachane na hilo Mada inaishia hapa nitawasimulia hadithi ili tumalizie muda uliobaki “.

Kila mtu alivutiwa.

“Jana usiku nilijitahidi kulala, lakini usingizi ulikuwa mbali na macho yangu, kwa hivyo nilifikiri bora nijaze petroli kwenye gari langu, nisipoteze wakati wangu kitandani alafu asubuhi ndio nipate usingizi.

Baada ya kujaza mafuta kwenye tanki langu, nilianza kuzurura katika eneo hilo, huku nikifurahiya amani ya kusafiri bila kusumbuliwa na trafiki.
Ghafla, kwenye kona nikamwona msichana mdogo mrembo ni mdogo sawa na nguo alizokuwa amevaa.
Lazima alikuwa anarudi kutoka disco au sherehe.

Kwa heshima, niligeuza gari langu kuelekea kwake na kumuuliza ikiwa ninaweza kumpa msaada wowote.
Aliniomba akasema atafurahi kama ntamuacha nyumbani kwao, nilikubali.

Alikaa kwenye kiti cha mbele na mimi.
Tulianza kuongea, na nilimshangaa alikuwa mwerevu sana, alikuwa anajua kujenga hoja na mada nyingi ambazo vijana wengi hawana.

Tulipofika nyumbani kwao, alikiri kwamba nina tabia njema na naheshimu wanawake alikili kwamba ananipenda.

Nilimkubalia kutokana na akili na uzuri wake hatamimi nimeanza kumpenda.
Nilimwambia juu ya kazi yangu kama profesa katika chuo kikuu.

Msichana aliniomba namba yangu, ambayo nilimpa kwa hiari.
kisha akaniomba jambo moja, ambalo ni singeweza kukataa kawaida.
Alisema kuwa kaka yake ni mwanafunzi katika chuo kikuu hapa, na akaniombaa nimtunze vizuri, kwani tutakuwa na uhusiano wa kudumu.

Nikamuomba jina la huyo mwanafunzi.
Alisema kuwa nitamtambua kwa ubora wake mashuhuri sana, Ni mpiga filimbi anapiga vizuri sana!
Macho yote darasani yakamgeukia yule kijana aliyepiga filimbi.

Profesa akasema:

“Aisee Sikununua Ph.D yangu kwa wana Saikolojia ..
Nimepata kwa kusoma. ” Hey! Toka nje wewe mpumbavu mjinga “🤣🤣🤣😂😂

MWISHO

Credit:Unknown

Msomeni blog: Facebook page 

Stori zaidi: Bonyeza hapa

Related Posts

Msomeni Blogu

Najihusisha na masuala ya kimtandao, mbinu mbalimbali za kuanzisha na kuendeleza biashara ya mtandaoni. Email yangu ni msomeniblogu@gmail.com au WhatsApp namba ni 0718453258

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

© 2021 MSOMENI BLOG - Theme by WPEnjoy · Powered by WordPress