Kama unataka kuwa na furaha epuka mambo haya

Kuwa na furaha ni jambo la muhimu sana kwa maisha yetu ya kila siku, inapokosekana furaha hupelekea mvurugano wa mambo na hata uvunjifu wa amani. Furaha haiji tu yenyewe ni lazima kufanya baadhi ya mambo na kuepuka mambo mengine ili kupata furaha.

Kufanya mambo ya furaha hutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine. Kila mtu ana mambo yake yanayompatia furaha. Mfano kuna watu furaha yao ni mziki, mpira wa miguu, muvi, ngono n.k Mahitaji muhimu kwa maisha ya geto

Ila kuna mambo ukiyafanya ni lazima upoteze furaha. Mambo haya ni ya kuyaepuka usiku na mchana. Baadhi ya mambo hayo ni kama ifuatavyo:

1. Kutaka kuwa sahihi kwa kila jambo

Kuwa sahihi

“Hakuna binadamu mkamilifu” ni msemo maarufu sana wenye ujumbe tosha kuwa kila mtu ana mapungufu yake hivyo huwezi kuwa sahihi katika kila jambo. Kufikiria jinsi ya Kuwa sahihi kwenye kila jambo ni sumu hatari sana inayoweza kuua furaha yako. Fanya jambo kwa uwezo wako na pale unapokosea pokea marekebisho na ufanye maboresho.

2. Kufikiria mambo yaliyopita

mawazo

“Yaliyopita si ndwele tugange yajayo” ni methali iloyobeba ujumbe mzito katika furaha ya mwanadamu. Kufikiria sana mambo yaliyopita yanachochea visasi, yanakosesha raha na yanatia hasira. Jikite katika kufikiria leo yako ikoje na utawezaje kuboresha kesho yako. Fanya haya kila siku kufikia mafanikio

3. Kukataa mabadiliko

Kuwa na furaha

Kukataa kubadilika ni chanzo hatari sana cha kukosa furaha. Pokea mabadiliko, kubali kubadilika, hukuzaliwa hivyo. Ni mwili na akili yako vilikubali mabadiliko na ndio maana leo umekua mkubwa. Linapotokea jambo lisilo la kawaida kubali kibadilika na uachane nalo. Karibisha hali mpya ya maisha.

Like page ya msomeni blog Facebook

4. Kujikatia Tamaa

Kujikatia tamaa

Epuka kujikatia tamaa mapema, kama jambo linakushinda jifunze kwa walioweza. Kujikatia tamaa na kuona kila jambo kwako ni gumu hukosesha furaha kwani kukufanya muda wote ujione kuwa ni mtu dhaifu usiyeweza kufanya jambo lolote. Jinsi ya kutengeneza blog ya WordPress bure

5. Kusubiri watu wakupongeze

Pongezi

Wahenga walisema “Tenda wema nenda zako usisubiri malipo”. Huu msemo una maana kubwa sana katika furaha yako. Usipende kusubiri watu wakupongeze kwani sio kila mtu anafurahishwa na mazuri unayofanya. Wapo watu kazi yao ni kuondoa thamani ya matendo ya watu wengine. Unayempenda hakupendi sababu zote hizi hapa

MWISHO

Related Posts

Msomeni Blogu

Najihusisha na masuala ya kimtandao, mbinu mbalimbali za kuanzisha na kuendeleza biashara ya mtandaoni. Email yangu ni msomeniblogu@gmail.com au WhatsApp namba ni 0718453258

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

© 2021 MSOMENI BLOG - Theme by WPEnjoy · Powered by WordPress