Jinsi ya kuuza bidhaa mtandaoni kwa haraka

Katika mwongozo huu utapata kufahamu njia rahisi na nyepesi za kuuza bidhaa mtandaoni kwa haraka bila ya kutoa jasho. Njia hizi zitakuwezesha kuuza bidhaa zako sehemu yoyote ndani ya Tanzania.

Kwa miaka ya hivi karibuni watumiaji wa internet wamekuwa wakiongezeka nchini Tanzania, hivyo kufanya biashara ya mtandaoni kukua kwa kasi. Wafanya biashara wameweza kutanua wigo wa wateja kutoka sehemu mbalimbali ndani ya nchi kwa kutumia internet.

Njia 4 za kuuza bidhaa mtandaoni kwa haraka popote Tanzania

1. Tumia mitandao ya kijamii

Kuuza bidhaa mtandaoni Facebook

Mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, Instagram na WhatsApp imekuwa na watumiaji wengi sana kutoka Tanzania, hivyo ni sehemu sahihi ya kutangaza bidhaa yako. Jiunge na mitandao hii kisha anza kupost bidhaa zako.

Jinsi ya kupost bidhaa: Andika maelezo ya kuvutia kuhusu bidhaa yako kisha ambatanisha na picha bila kusahau kuweka bei ya bidhaa na sehemu unayopatikana. Pia andika namba yako ya simu. Tuma bidhaa yako kwenye magrup ya WhatsApp, magrup ya Facebook na kwenye akaunt yako.

2. Tuma bidhaa kwenye website za kuuza na kununua

Kuuza bidhaa mtandaoni Jiji

Kuna websites nyingi ambazo unaweza kupost bidhaa yako na baada ya muda mfupi ukapata wateja. Websites hizi ni kama vile Jiji, Kupatana, zoom Tanzania na msomeni blog.

3. Kufungua duka la mtandaoni

Biashara ya mtandaoni Tanzania

Kufungua duka la mtandaoni ni jambo la dakika chache tu. Unaweza kufungua bure au kwa gharama nafuu. Utaweza kupost bidhaa zako na wateja wakaweka oda na kulipia kabisa. Hii ndio njia inayotumiwa na wauzaji maarufu wa mtandaoni kama alibaba, Kikuu, Amazon n.k. Maduka 4 bora ya kununua bidhaa mtandaoni-Tz

Jifunze hapa Jinsi ya kuanzisha duka la mtandaoni bure

4. Matangazo ya kulipia

Facebook ads

Hii ni njia ambayo unahitaji bajeti ili kufanikisha. Unaweza kujiunga na huduma ya kulipia tangazo lako ili liwe sponsored na liweze kusambazwa kila kona ya nchi. Baadhi ya huduma bora za kulipia tangazo lako ni Facebook, Google ads na Instagram.

MWISHO

Kwa maswali na msaada tuandikie chini kwenye comment au bonyeza hapa

 

Related Posts

Msomeni Blogu

Najihusisha na masuala ya kimtandao, mbinu mbalimbali za kuanzisha na kuendeleza biashara ya mtandaoni. Email yangu ni msomeniblogu@gmail.com au WhatsApp namba ni 0718453258

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

© 2021 MSOMENI BLOG - Theme by WPEnjoy · Powered by WordPress