Jinsi ya kutengeneza blog ya WordPress bure

WordPress ni miongoni mwa platform maarufu ulimwenguni kwa utengenezaji wa blogs na websites. Katika ulimwengu wa leo, kutengeneza blog ya WordPress ni wazo zuri sana kwani asilimia 90 ya blog zote duniani zimetengenezwa na WordPress.

Blog au website za WordPress ni nzuri kutokana na uwezo wake wa kufit kila aina ya blog kama vile biashara, habari na matukio, michezo na aina nyingine za blog.  Hii ni kutokana na uwepo wa plugins nyingi zinazosaidia kutengeneza blog yako vile unataka.

Katika post hii utajifunza jinsi ya kutengeneza blog ya WordPress bure au kwa gharama ndogo ya tsh 25,000/.

Kabla ya kuanza hatua ya kwanza unatakiwa kufahamu mambo yafuatayo:

1. Domain name: Hii ni link ya blog yako mfano www.blogyangu.com au msomeni.co.tz. Domain name unaweza kupata bure ila inakuwa ni sub-domain mfano www.blogyangu.wordpress.com au unaweza kununua domain kwa shilingi 25,000 hadi 30,000 kwa mwaka kutoka kwa wauzaji wa domain. Hapa Tanzania wauzaji wazuri wa domain ni Dudumiz

Kutengeneza blog ya WordPress-nunua domain name
Unaweza kuchagua domain kama vile.co.tz au .com kulingana na bajeti yako. Faida ya kuwa na domain ya kulipia ni kuifanya blog yako iwe professional na kukubaliwa na Google (AdSense) kuweka matangazo kwenye blog yako. Google hawakubali kuweka matangazo kwenye domain ya bure.

Kama unahitaji kununua domain name bonyeza hapa ila kama unahitaji kuanza na domain ya bure endelea chini.

2. Hosting: Hii ni sehemu ambayo blog yako inawekwa. Yaani kila kitu kwenye blog yako kama vile picha, posts, videoa n.k vinatunzwa katika Hosting. Kupata hosting ya bure inawezekana ila huwa zina changamoto kama vile blog yako kuzima ghafla, haupati msaada wowote endapo blog yako imepata tatizo na blog yako kuwa chini (haiload)  mara kwa mara.

Kwa hapa Tanzania hakuna hosting ya bure ila Ukinunua hosting unapata domain bure. Gharama ya hosting inaanzia tsh 40,000/ kwa mwaka (unalipia kila mwaka).  Tazama hosting na gharama zake hapa. Kupata hosting ya bure endelea chini 

Jinsi ya kutengeneza blog

Baada ya kufahamu mambo hayo mawili tuendelee na hatua ya kwanza.

Jinsi ya kutengeneza blog ya WordPress hatua kwa hatua

1. Fungua akaunti kwenye googiehost

Googiehost ni miongoni mwa web hosting na wauzaji wa domain name. Googiehost wanatoa ofa ya hosting ya bure na domain ya bure. Pia kama tayari una domain name yako watakupatia hosting bure. Kwanini googiehost? Sababu ni iko fasta, hakuna tatizo la blog kutokuwa hewani na unapata ulinzi wa blog yako yaani SSL bure. Epuka hosting za bure kama vile infinity free, byethost, freehosting.com na awardspace.

Ukishajisajiri kwenye googiehost itachukua hadi siku tatu akaunti yako kuthibitishwa. Fuata hatua zifuatazo

i) Bonyeza hapa kuingia googiehost

ii) Shuka chini kisha bonyeza Get for free

Googiehost host

3. Bonyeza sehemu iliyozungushiwa kama unahitaji domain name ya bure kama vile blogyangu.cu.ma au sehemu ya juu yake kama ulisajiri domain name ya kulipia. 

Googiehost free account

Utaandika domain unayotaka kulingana na mapendeleo yako. Onyo: Hili sio jambo la kujaribu, fikiria kwanza kabla haujachagua domain ya kuandika kwani hautaweza kubadilisha. Usijejuta baadae.

4. Bonyeza Check baada ya kuandika domain yako. Katika ukurasa unaofuata andika neno I want to start my first blog kisha weka tiki sehemu iliyoandkiwa free speed and security optimisation.  Kisha Shuka chini bonyeza neno Continue

Googiehost

5. Jaza taarifa zako kwenye fomu kisha bonyeza Complete order na baada ya hapo utatakiwa kusubiri masaa 24 hadi siku tatu akaunti yako kukubaliwa.

Baada ya akaunti yako kukubaliwa endelea na hatua ya Pili kama ifuatavyo. 

2. Anza ku-install WordPress kwenye akaunti yako ya googiehost.

⛔ Login kwenye akaunti yako ya googiehost hapa.

Ukishalogin Shuka chini kisha bonyeza sehemu iliyoandkiwa Services

Googiehost service

⛔ Shuka chini kisha bonyeza Manage product

Googiehost service

⛔ Katika ukurasa unaofuata bonyeza One click login kisha bonyeza direct admin

Googiehost

⛔ Bonyeza alama ya menu juu upande wa kulia

Googiehost

⛔ Shuka chini kisha bonyeza WordPress. Ikifunguka Utaandika taarifa za msingi za blog yako kama vile password, username na  jina la blog yako kisha bonyeza install

Googiehost

⛔ Ikishakamilika ku-install WordPress,

Googiehost

Baada ya hapo blog yako itakuwa iko live kwenye internet. Ingia kwenye tab nyingne au bonyeza juu ya browser sehemu ya andika link ya website kisha andika link au domain name yako alafu ongeza neno /wp-admin mbele ya domain name yako. mfano: blogyangu.cu. ma/wp-admin baada ya kufunguka

Msomeni.co.tz

andika username na password ulizoandika wakati unajaza kabla ya ku-install WordPress, kwenye hatua ya hapo juu.  (sio ulizoandika wakati unajiunga na googiehost) 

⛔ Ukishalogin utakuwa umeingia kwenye dashboard ya WordPress bonyeza sehemu ya menu juu kushoto (kama unatumia simu)

Kutengeneza blog ya WordPress

shuka chini kisha bonyeza sehemu  iliyoandkiwa Appearance alafu bonyeza theme,  chagua theme yenye muonekano mzuri wa blog unayotaka (theme ni muonekano mzima wa blog yako, hii ndio Inafanya blog yako iwe na mwonekano mzuri au mbaya)

Msomeni.co.tz

⛔ Ukishachagua theme unayotaka utabonyeza install kisha activate. Bonyeza neno linalofuata baada ya appearance ambalo ni plugins ku-install plugin za muhimu kama vile jetpack, yoast, wp fastest cache n.k.

⛔ Andika posts, ongeza pages na mambo mengine mengi yanapatikana kwenye dashboard ya WordPress.

MWISHO

Kama una maswali au unahitaji msaada wasiliana nasi WhatsApp. Bonyeza hapa

Related Posts

Msomeni Blogu

Najihusisha na masuala ya kimtandao, mbinu mbalimbali za kuanzisha na kuendeleza biashara ya mtandaoni. Email yangu ni msomeniblogu@gmail.com au WhatsApp namba ni 0718453258

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

© 2021 MSOMENI BLOG - Theme by WPEnjoy · Powered by WordPress