Jinsi ya kutengeneza blog-(hatua kwa hatua)

Katika mwongozo huu, nitakuonyesha jinsi ya kutengeneza blog nchini Tanzania kwa urahisi (na kwenye bajeti). Hakuna uzoefu wa kiufundi unaohitajika. Ni rahisi na kwa kasi zaidi kuliko unavyofikiria!

Ni wazi kwamba intaneti imekua ikitengeneza maelfu ya fursa kwetu kwa hiyo, sekta ya blogu pia inakua kwa kasi nchini Tanzania. Kwa ufupi, Blogging inakuwa chaguo kamili la kazi za ujasiliamali kwa vijana siku hizi

Kwa kuongezea, blogu zina uwezo mkubwa zaidi katika kukuza biashara ya mtandaoni lakini wakati mwingine watu hukwama kutokana na ukosefu wa maarifa ya kiufundi.

Walakini, si kweli kwamba unahitaji kuwa mtaalamu kuanza au kuunda blogu. Unahitaji tu kufuata hatua hizi na utaanzisha blogi yako kwa urahisi ndani ya dakika 15.

Jinsi ya kutengeneza blog yako ya Kwanza

Sasa unaweza kutengeneza blogu yako bure au kwa bajeti ndogo ya kuanzia kiasi cha Tsh 25,000 hadi 40,000/- kwa mwaka.

Hizi ni hatua kwa hatua jinsi ya kutengeneza blog yako ya kwanza na ukaitumia kutengeneza bland au pesa kila siku

Hatua ya 1: Kuchagua CMS sahihi

Hatua ya 2: Kuchagua Domain sahihi ya blog

Hatua ya 3: Kuchagua Mtoaji Bora wa hosting service

Hatua ya 4: Kuanzisha Blog

Hatua ya 5: Kudizain Blog yako

Hatua ya 6: Anza Kupata pesa

Hebu tuchimbue kwa kina katika kila moja ya hatua hizi.

Hatua ya 1: Kuchagua CMS sahihi

CMS or Content Management System. CMS au Mfumo wa Usimamizi wa Maudhui kimsingi ni platform za blogu kama vile Blogspot, WordPress, Drupal, Joomla, Wix, AinaPad nk ambapo utaweka faili zako zote za blog yako. Kati ya platform zote za blogu tutatumia WordPress kwa sababu  zifuatazo.

  1. Ni bure.
  2. Ni rahisi sana kudizaini blogu na kuelewa dashibodi yake.
  3. WordPress ina zaidi ya themes 5000+ za bure na za kulipia.
  4. Hivi sasa kuna zaidi ya Plugins za bure zaidi ya 70,000 zinazotolewa na WordPress kuendesha blogu yako haraka na kwa ufanisi.
  5. Pia, kuna jukwaa la WordPress ambalo wanaweza kukusaidia chochote unachohitaji wakati wa kuendesha blogu yako. Jiunge na Jukwaa lao la WordPress

Asilimia 98% ya blogu zote ulimwenguni kwa sasa zinatumia WordPress. Hata mimi pia ninatumia WordPress kwa blogu zangu zote ikiwa ni pamoja na blogu hii ya msomeni ya blogu. Hivyo ninapendekeza kwa nguvu zote kuunda blogu yako kwa kutumia WordPress CMS.

Hatua ya 2: Kuchagua Domain name sahihi ya blog

Hatua ya 2 ni muhimu sana kwa sababu jina la domain yako litaonyesha niche (blog inahusu nini) ya blogu yako. Kwa hivyo lazima uitendee haki blogu yako kwa kuchagua domain name sahihi inayoendana na maudhui ya blog yako.

Blogu yangu https://msomeni.co.tz yote ni juu ya vidokezo vya elimu na maarifa kama jina linavyoonyesha.

Ikiwa unapanga kuanzisha blogu yenye kuhusu Mpira wa Miguu au muziki basi chagua majina kama musictrends.co.tz au SoccerFan.com.

Bila shaka umeshapata idea

Yafuatayo ni mambo machache unayopaswa kukumbuka.

#1 jina la domain lazima liendane na madhumuni ya blogu yako.

#2 lazima liwe rahisi kukumbuka na kutamka.

#3 Tumia .com. Ikiwa umekosa .com basi jisikie huru kuchagu nyingine  kama .in, .org, .net, .info, .co.tz nk

#4 Epuka kutumia namba na kistari katika domain ya blog yako.

Hatua ya 3: Kuchagua Mtoaji Bora wa hosting service

WordPress ni programu tu ambayo unaunda blogu kwa kuweka faili zote muhimu za blog yako. Lakini utahifadhi wapi blogu yako? Naam ndivyo unavyohitaji mtoa huduma wa hosting?. Hosting hufanya kazi ya huhifadhi maudhui yako yote ya blogu yako kama faili za html, faili za css, picha, video nk mahali pamoja na kuifanya ipatikane kwenye intaneti.

Kwahiyo unahitaji mtoa huduma bora ya hosting ili kuweza kuhifadhi blog yako na kuifanya ipatikane duniani kote. Lakini ni mtoa huduma gani ya hosting utachagua? Kwa miaka 5 nimetumia na kupata uzoefu juu ya ubora ya watoa huduma hizi. Hivyo mmoja wa watoa huduma wa kuaminika zaidi nchini Tanzania ni Duhosting.

Miongoni mwa huduma nzuri zinazotolea na duhosting ni huduma ya usaidiza wa haraka, gharama nafuu ukilinganisha na watoa huduma wengine na pia unapata domain name bure.

Hatua ya 4: Kutengeneza blog yako na Duhosting

Gharama za kuanzisha blog kwa kutumia duhosting ni Tsh 80,000 au 40,000 kwa wanafunzi. Pia unaweza kusajili domain name kwa Tsh 22,000 kwa mwaka.

  1. Tembelea Duhosting hapa.
  2. Chagua kifurushi unachotaka kujiunga

webhosting in tanzania

Unaweza kufanya malipo kwa kutumia Tigo Pesa, M-Pesa or Airtel Money

Baada ya kukamilisha malipo ingia kwenye huduma uliyolipia kisha nenda kwenye cpanel (follow this guide on how to install wordpress in cpanel)

Hatua inayofuata baada ya kukamilisha kuinstall wordpress kwenye cpanel unaweza kulog in kwenye wordpress kwa kuandika /wp-admin mbele ya domain yako  kwa mfano yourdomain.com/wp-admin)

Sasa utaingia kwenye dashbodi y wordpress na hapa ndipo utaanza kuunda maudhui ya blog yako kama vile kuweka post, kudizaini mwonekano wa blog na mambo mengine mengi

Jinsi ya kutengeneza blog ya WordPress

Now use all the powerful yet simple to use WordPress features to transform your blog into a masterpiece.

Hatua ya 5: Kudizain Blog yako 

Haya ni mambo ya muhimu katika kudizaini mwonekano wa blog yako.

1. Install a theme

Theme ni sehemu muhimu sana katika blog yako. inakufanya uweze kubadilisha mwonekano au kubuni mtindo na mpangilio wa blog yako. Kuna maelfu ya themes za bure na za kulipia zinazopatikana kwenye WordPress.

Jinsi ya kubadilisha theme ingia ‘Appearance‘ kisha bonyeza themes (tazama picha ya dashbodi hapo juu). Bonyeza ‘Add New’ utaona maelfu ya themes, utachagua unayoona inafaaa kwa blog yako.

2. Install Plugins muhimu

Plugins za WordPress ni kama programu ambazo zinakusaidia kuongeza vipengele zaidi kwenye blog yako na kuifanya iwe na ufanisi zaidi na haraka. Lazima ku-install baadhi ya plugins muhimu za kuanzia kwenye blog yako. Bonyeza ‘Plugins’ (tazama picha juu) na kisha bonyeza ‘Add New‘ ku-install plugins.

Baadhi ya plugins muhimu ni pamoja na Yoast SEO, JetPack, Contact Form 7, Akismet, Classic Editor, WP Super Cache, Smush Image Compression.

3. Andika post yako ya kwanza

Ili uwe blogger mzuri unatakiwa uandike angalau post mbili hadi tati kwa wiki. Hii ni kuifanya blog yako iwe active kwa wasomaji wako. Katika kuandika post hakikisha maneno yanaanzia 800 na kuendelea.

Pia epuka kukopi post za blog nyingine kwani hupunguza matamanio ya wasomaji. Jikite katika kuandika post za kipekee zenye vichwa vya habari vyenye kuvutia.

Hatua ya 6: Anza Kupata pesa

Blog inakuwa kazi maarufu sana ya wakati wote nchini Tanzania na duniani kote. Mamilioni ya wanablogu wanaingiza $1000 hadi $100,000 kwa mwezi kutoka kwenye blogu zao.

Kama unahitaji kuingiza pesa ya kutosha kupitia blog yako unatakiwa kuwa serious ambapo inabidi utumie masaa 3 hadi 6 kwa siku kushughulikia blog yako ikiwa ni pamoja na kupromoti blog yako kwenye mitandao ya kijamii, kuwajulisha marafiki kuhusu blog yako na kufanya interview kwenye media mbalimbali ili kuitangaza blog yako

Kuna mambo mawili ya kutilia mkazo ili uweze kupata watumiaji wengi wa blog yako

  1. Maudhui
  2. SEO (Search Engine Optimization)

Jikite katika kuandika maudhui yaliyo bora kama vile kuelimisha, kutatua changamoto mbalimbali za jamii, kuburudisha nk. Ukiweza kupata watu wengi kwenye blog yako hapo utaanza kuweka matangazo mbalimbali kama vile matangazo ya google (Adsense). Pia blog yenye watumiaji wengi huvutia wawekezaji mbalimbali kutangaza biashara zao hivyo jikite katika kuandika maudhui halisi na yenye kuvutia ili kuvutia wasomaji wengi zaidi na kuanza kuingiza pesa kupitia blog yako.

Hitimisho

Kazi ya blogging ni kazi kama kazi zingine ambapo unatakiwa kuwa na mipango madhubuti ili kufanikisha malengo yako. Mwanzo huwa ni mgumu lakini matunda yake ni matamu sana. Pili, usifanye kazi ya blog kwa kujifurahisha wakati wengine wnapiga pesa, jikite katika kuandika maudhui ya pesa.
KILA LA KHERI

 

Related Posts

Msomeni Blogu

Najihusisha na masuala ya kimtandao, mbinu mbalimbali za kuanzisha na kuendeleza biashara ya mtandaoni. Email yangu ni msomeniblogu@gmail.com au WhatsApp namba ni 0718453258

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

© 2021 MSOMENI BLOG - Theme by WPEnjoy · Powered by WordPress