Jinsi ya kumuweza demu mpenda pesa

Kuwa kwenye Mahusiano na demu au mwanamke anayependa pesa ni sawa na kuajiri mtu unayemlipa kila mwezi. Sio kazi ndogo kumudu matumizi ya wanawake wa aina hii hata kama una pesa za kutosha.

Wanadamu huwa tuna tabia ya kuweka mipango au bajeti ya matumizi yetu na kila mpango huwa na kikomo cha matumizi. Ikitokea mwanamke anaomba pesa kila kukicha anakuwa ni kero kwa sababu itakulazimu kutumia pesa nje ya mipango yako. Na Ukiwa hauna pesa kabisa inakuwa tatizo zaidi.

Kiukweli sio jambo zuri kumnyima pesa mwanamke hasa akiwa hana kazi ya kuingiza kipato lakini kuomba pesa mara kwa mara anakutoa kwenye ramani ya matumizi yako.

Mpe pesa mwanamke

Ikiwa upo kwenye mahusiano na mwanamke anayependa sana pesa na wewe umeichoka tabia hii na hauna jinsi ya kumuepuka kwasababu bado unampenda hata kama yeye hakupendi unatakiwa kufanya mambo kadhaa na tabia yake ya kuomba pesa itakuwa imekoma.

Fanya yafuatayo kumkomesha mwanamke mpenda pesa

1. Weka ahadi feki

Mpe mwanamke pesa

Hii ni mbinu inayofanya kazi vizuri sana katika kumtuliza mwanamke anayependa pesa. Unachotakiwa kufanya ni kwamba pindi anapokuomba pesa usimwambie hauna ila mpe ahadi ya kumpa baada ya siku kadhaa mfano baada ya wiki moja utampatia kiasi chote alichoomba.

Unayempenda hakupendi sababu zote hizi hapa

Kabla ya siku uliyomuahidi haijafika mnunulie zawadi yoyote ya pesa ndogo unayoweza kuimudu kisha mpatie na mwambie kuwa ile pesa uliyomuahidi kumpa hautaweza kumpatia kwa siku uliyoahidi ila utampatia siku chache mbele lakini usitaje ni siku gani ila mpe moyo.

2. Mpe mpango wa kumnufaisha

Mpe mwanamke pesa

Unatakiwa uandae mpango au mipango ya kubuni inayolenga kumnufaisha yeye na maisha yake kwa ujumla ili atakapoomba pesa mkumbushe kuwa pesa unaweka kwa ajili ya mpango uliopanga na ukiwa unatoatoa pesa ovyo mpango hautakamilika. Hii itamfanya apunguze kuomba pesa ili lengo alilopangiwa likamilike. Unaweza kuandaa mpango kama vile kumnunulia simu mpya au chochote kile yeye anapenda.

3. Jifanye hauwezi kutunza pesa

Kuweka au kutunza pesa inahitaji moyo wa uvumilivu sana ili kujiepusha usitumie hovyo. Sasa jifanye wewe hauwezi kutunza pesa badala yake uwe unampa yeye kiasi kidogo cha pesa awe anakitunza kwa ajili ya matumizi ya baadae.

Kutunza pesa

Kwa jinsi atakavyokuwa anaona pesa unayompa atunze ni ndogo atakata tamaa kuomba na kujua kuwa mambo yako hayajakaa sawa hivyo ataanza kuwa mvumilivu na kusubiri hadi mambo yako yakae sawa. Usiache kufatilia pesa unayompa atunze.

Njia 10 za kuwa na uume mkubwa

4. Mwambie akupe jumla ya matumizi yake yote

Ili asiweze kuharibu bajeti zako,  mwambie akupe orodha ya matumizi yake yote ya mwezi mzima na jumla ya pesa itakayogharimu. Hii itakusaidia kujua ni matumizi gani ya lazma na yasiyo ya lazma na kukadilia kiasi cha pesa utakachompa au usimpe kabisa ndani ya muda fulani.

5. Mpe pesa bila yeye kutegemea au kuomba

Mpe mwanamke pesa

Hautakiwa kumnyima moja kwa moja, ila mpe kulingana na kile unapanga wewe kimpa na sio anachoomba yeye kwa sababu hawa watu huwa hawaishiwi matumizi. Cha kufanya andaa kiasi cha pesa kulingana na bajeti yako kisha mpe bila yeye kuomba.

Jinsi ya kutengeneza blog-(hatua kwa hatua)

Hii itakusaidia kupanga bajeti zako vizuri,  hata akiomba pesa kipindi hautaki kumpa utamwambia tu mambo hajakaa sawa kwasababu yeye mwenyewe ni shahidi maana mambo yakiwaga sawa huwa unampa tu hata kama hajaomba. Jifanye unaelewa sana matumizi yake, na unajali matumizi yake kwahiyo unapopata pesa tu lazima umpe. Ataamini kwasababu huwa unampa bila yeye kuomba.

MWISHO.

Related Posts

Msomeni Blogu

Najihusisha na masuala ya kimtandao, mbinu mbalimbali za kuanzisha na kuendeleza biashara ya mtandaoni. Email yangu ni msomeniblogu@gmail.com au WhatsApp namba ni 0718453258

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

© 2021 MSOMENI BLOG - Theme by WPEnjoy · Powered by WordPress