Jinsi ya kuanzisha duka la mtandaoni bure

Kuanzisha duka la mtandaoni ni kazi ya dakika chache tu ambapo utaweza kuanzisha duka lako na kupost bidhaa zako kwa kutumia smartphone yako. (Sio lazima uwe na laptop au computer)

Biashara ya mtandaoni kwa siku za karibuni imekuwa ikikua kwa kasi sana kutokana na ongezeko la wauzaji na wanunuaji wa mtandaoni. Ugonjwa wa corona imekuwa sababu moja wa kukuza biashara ya mtandaoni kutokana na lockdown iliyopelekea watu kuagiza bidhaa mtandaoni. Maduka 4 bora ya kununua bidhaa mtandaoni-Tz

Katika post hii utapata kujifunza hatua kwa hatua jinsi ya kufungua duka lako la mtandaoni na kuanzia kupokea oda kutoka kwa wateja sehemu mbalimbali ndani ya Tanzania.

Hatua za kuanzisha duka la mtandaoni

1. Tengeneza blog au website.

Hii ni hatua muhimu sana ambapo unatakiwa uwe na website yako ambayo ndio itakuwa stoo au duka lako. Hapa blog inayofaa ni blog iliyotengenezwa kwa kutumia WordPress. Jifunze jinsi ya kutengeneza blog ya WordPress bure.

2. Install woocommerce plugin

Baada ya kutengeneza blog yako ya WordPress unatakiwa ku-install plugin ya woocommerce.

Woocommerce ni plugin maalumu kwa kuanzisha duka la mtandaoni. Plugin hii ni bure. Unaweza kutumia kupokea oda kutoka kwa wateja au wateja kulipia bidhaa moja kwa moja.

3. Install theme nzuri kwa duka lako

Kuna themes nyingi sana ambazo zitaonesha mwonekano mzuri wa duka lako. Mfano ni hii theme shopping cart

Theme ni mwonekano wa blog yako. Kama blog yako ni ya biashara inabidi iwe na mwonekano wa kibiashara. Tumia theme inayoendana na blog yako. Zipo themes nyingi sana za kibiashara.

Biashara ya mtandaoni Tanzania- kuanzisha duka la mtandaoni

4. Fanya setting za plugin ya woocommerce

Anza kufanya setting katika plugin ya woocommerce kama vile kuweka anuani ya duka lako, kuseti pesa ya kutumia mfano dola au shiling ya Tanzania.

5. Post bidhaa zako

Ni wakati sasa wa kupost bidhaa zako baada ya kumaliza kufanya setting muhimu. Ingia upande wa kushoto wa dashboard ya WordPress sehemu iliyoandikwa Product kisha add new kuanzia kupost bidhaa zako.

6. Sambaza au Tangaza duka lako

Ingia kwenye mitandao ya kijamii na uanze kusambaza link ya duka lako. Angalizo: epuka kusambaza link mara nyingi kwa wakati mmoja kwenye Facebook kwasababu link yako itafungiwa na hautaweza kuipost popote Facebook.

Angalizo: Ni lazima uwe umetengeneza blog yako kwwnye WordPress. Kuelewa zaidi bonyeza hapa

MWISHO

Kwa msaada zaidi wasiliana nasi hapa

Related Posts

Msomeni Blogu

Najihusisha na masuala ya kimtandao, mbinu mbalimbali za kuanzisha na kuendeleza biashara ya mtandaoni. Email yangu ni msomeniblogu@gmail.com au WhatsApp namba ni 0718453258

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

© 2021 MSOMENI BLOG - Theme by WPEnjoy · Powered by WordPress